
Staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amefunguka sababu za kuwaondoa Juma jux na Darassa katika orodha ya wasanii watakao kuwepo kwenye Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL ambalo litafanyika machi 5 mwaka huu.
Kwenye mkao na Waandishi wa habari nchini Tanzania, Harmonize Anasema hayo yalitokea kutokana na Kutokuwa na mawasiliano mazuri baina ya Uongozi wake na uongozi wa Mastaa hao, huku akisema kuwa hakuna ugomvi wowote kati yake na Msanii juma jux pamoja Darassa, Hivyo watu wasikuze vitu.
Sanjari na hilo Harmonize ametoa ofa ya watu 1000 wa kwanza kununua Tiketi za kuudhuria katika Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL ambapo tiketi zitaanza kuuzwa rasmi siku ya tarehe 15, hivyo watapata tiketi kwa Shilingi elfu 5 za Kitanzania.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amesisitiza kuwa idadi ya wasanii watakao kuwepo kwenye Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL bado itaendelea kutangazwa ikizingatiwa kuwa mpaka sasa ni wasanii 43 ambao wameshatangazwa kumsindikiza harmonize kwenye tamasha lake.