
Mwanamuziki Winnie Nwagi ni moja kati ya watu ambao wanazungumza kilicho akilini mwao bila kushurutishwa na mtu yeyote. Lakini pia huwa anawajibu wakosoaji wake bila uwoga wotewote.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Kwata Essimu amewatolea uvivu mashabiki zake wa Dubai ambao juzi kati walimshambulia baada ya kudinda kupiga nao picha.
Kulingana na mashabiki hao, Winnie Nwagi alikataa kupiga nao picha baada ya kusafiri mwendo mrefu kwenda kumuona hotelini.
Sasa kupitia video aliyoichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii winnie nwagi amesema ana haki ya kutopiga picha na mashabiki hivyo mashabiki wanapaswa kujifunza kuwaheshimu wasanii.
Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa hajutii kitendo cha kukataa kupiga picha na mashabiki huku akiwataka wanaomkosoa kwa hatua yake hiyo washughulike na maisha yao.
“Simuogopi mtu yeyote isipokuwa Mungu, Hauna sababu ya kushurutisha kupiga picha nami,” alisikika kwenye audio clip inayosambaa mitandaoni.
Utakumbuka Winnie Nwagi amekuwa akikosolewa kila mara na mashabiki wa muziki nchini Uganda kutokana na mienendo yake inayokwenda kinyume na maadili ya jamii