Entertainment

MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MANABLOGU ROBERT ALAI

MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MANABLOGU ROBERT ALAI

Mahakama ya Milimani Jijini Nairobi imeahirisha kwa mara nyingine kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki Ringtone dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimshambulia na kumjeruhi vibaya mwaka wa 2021.

Akizungumza nje ya mahakama ya Milimani Wakili wa Ringtone Evans Ondiek amesema Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 9 mwezi mei mwaka wa 2022, siku ambayo mahakama itatoa mwelekeo.

Kwa upande Mwanamuziki Ringtone amesema ana imani kwamba mahakama itamtendea haki ikizingatiwa kuwa ana ushahidi wa kutosha dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimjeruhi vibaya kichwani kwa rungu.

Hii sio mara ya kwanza kesi hiyo kuaahirishwa mwezi Agosti mwaka jana iliahirishwa tena baada ya Mwanablogu Robert Alai kuachiwa kwa dhamana ya shillingi laki tatu za Kenya.

Utakumbuka Ringtone na Robert Alai waliingia kwenye ugomvi mwezi Julai mwaka wa 2021 baada ya wawili hao kuhusika kwenye ajali ya barabarani ambapo Ringtone alimtuhumu Alai kwa kumpiga Rungu ya kichwa na kuaharibu gari lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *