
Kundi la muziki nchini Sauti Sol limetangaza ujio wa ziara yao ya kimuziki Barani ulaya kwa kuanika mkeka wa mataifa ambayo watafanya shows.
Kupitia ukurasa wao rasmi wa instagram Sauti Sol, wameipa ziara hiyo jina la Sauti Sol Europe Tour na itaanza Aprili Mosi, mwaka wa 2022 huko Barcelona nchini Uhispania na itafanyika ndani ya miji 19 kwa kipindi cha mwezi mmoja..
Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Ujerumani, Ureno, Ufaransa, Denmark, Uingereza, Belgium ambapo kilele chake kitakuwa nchini Uholanzi Juni 28 mwaka wa 2022.