
Staa wa muziki nchini Masauti amekanusha tuhuma za kumuibia nguo za ndani, simu na hela mwanamke mmoja, mjini Mombasa.
Katika mahojiano yake hivi karibuni amesisitiza kuwa mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Bianca alikuwa na lengo la kumharibia jina huku akiweka wazi kuwa alikuwa anashinikiza kuondoka na Masauti katika ukumbi huo wa Burudani.
Kauli ya masauti imekuja mara baada ya kuandikisha taaarifa katika kituo cha polisi cha Nyali baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kama Bianca kudai kuwa msaani huyo alimwibia nguo za ndani (Chupi) simu na ksh 20,000 nje ya jumba moja la burudani eneo la Nyali.
Kwa mujibu walioshuhudia tuki hilo Februari 13 mwaka huu eneo Nyali,Mwanadada huyo alionekana akitolewa kwa lazima na Masauti nje yagari alilokuwa ameegesha nje ya ukumbi huo wa burudani huku mwanamke huyo akisistiza kuwa alipoteza vitu hivyo kwenye gari hilo.