Entertainment

MWANAMUZIKI WA TEAM NO SLEEP RAHMAH PINKY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

MWANAMUZIKI WA TEAM NO SLEEP RAHMAH PINKY AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Rahmah Pinky ameachia rasmi album yake ya kwanza chini ya lebo ya muziki ya Team No Sleep.

Album hiyo ambayo imepewa jina la Seven Teen ina jumla mikwaju 6 ya moto ambayo pinky amezifanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote.

Nyimbo ambazo zinapatikana kwenye album hiyo ya Pinky imeandikwa na wasanii Sama Sojah, Khalifa Aganaga, na Dokta Brain, huku maprodyuza kama Bushigntone, Nessim, na Chemical Beatz, wakihusika kikamilifu kwenye mapishi ya Audio.

Seven Teen album ina nyimbo kama, Onyuma Okulaba,Kukwagala, SuperStar, na inapatikana exclusives kwenye majukwaa yote kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.

Utakumbuka Rahmah Pinky mwenye umri wa miaka 17 alitambulishwa kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep mwishoni mwa mwaka wa 2021 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Sheebah Karungi ambaye alizinguana vibaya na meneja wake Jeff Kiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *