
Msanii nyota nchini Mejja kwa nyingine amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaotumia jina lake vibaya kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Kupitia ukurasa wake instagram Mejja amesema akaunti zote ambazo zinatumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter ni batili huku akiwataka mashabiki zake wawe waangalifu na matapeli wanaotumia chapa yake kujitakia makuu.
Kauli ya Mejja imekuja mara baada ya ukurusa mmoja kwenye mtandao wa twitter unaotumia jina lake kumwagia sifa diamond platinumz jambo ambalo lilipelekea ukurasa rasmi wa lebo ya wcb inayomilikiwa diamond kuchapisha ujumbe huo kwenye mitandao ya kijamii.
Hii sio mara ya kwanza kwa mejja kuwaonya watu dhidi ya akaunti feki zinazotumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter kwani mwaka wa 2020 alifanya hivyo tena mara baada ya jamaa mmoja kumtuhumu kuwa alidinda kutokea kwenye interview yake licha ya kumlipa shillingi elfu 12.