Entertainment

YKEE BENDA AWATAKA WASANII WA UGANDA KUTOKUBALI KUTUMIWA VIBAYA NA MAPROMOTA WA MUZIKI

YKEE BENDA AWATAKA WASANII WA UGANDA KUTOKUBALI KUTUMIWA VIBAYA NA MAPROMOTA WA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda amewataka wasanii wenzake kuanza kuwalipisha pesa nyingi mapromota wa muziki nchini humo ambao wanawaleta wasanii wa Nigeria kwenye shows zao.

Bosi huyo wa Mpaka Records amewataka wasanii wenzake kuwa na msamimo dhabiti dhidi ya mapromota hao ili waweze kuwalipa pesa sawa na wasanii wa Nigeria kwani wana uwezo wa kufanya hivyo.

Kauli ya Ykee Benda inakuja siku chache baada ya kuwataka mapromota muziki nchini Uganda kuwazingatia wasanii wa ndani kwenye shows zao badala ya kuwapa kipau mbele za wasanii wa nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *