
Female singer kutoka Kenya Nicah The Queen ametoa changamoto kwa wanawake wenzake kujishusha na kushirikiana na wapenzi wao wa zamani kuwalea watoto wao waliozaa nje ya ndoa badala ya kuendekeza kiburi na majivuno.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nicah The Queen amesema kiburi na majivuno imewaponza wanawake wengi na kuwafanya kuona utaratibu ulezi wa pamoja yaani, Co-parenting kuwa mgumu kwao jambo ambalo anadai limepelekea watoto wengi kukosa upendo wa baba katika maisha.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Na Wewe” amesema kila mtoto ana haki ya kupata upendo na mahitaji ya msingi kutoka kwa mama na baba mzazi licha ya utofauti wao.
Kauli ya Nicah The Queen imekuja mara baada ya kukutana baby daddy wake Dr. Ofweneke kwenye hafla ya kufuzu kwa mtoto wao ambapo walimuonyesha upendo licha ya kutengana na kuingia kwenye mahusiano mengine tofauti.