
Msanii wa kundi la Mbuzi Gang, Fathermoh amethibitisha kuwa wasanii kundi hilo walihusika kwenye Ajali ya barabarani Februari 26.
Fathermoh ameeleza hayo baada ya kuwepo na tetesi mitandaoni ambapo aliamua kuweka wazi suala hilo kupitia mtandao wa Instagram.
Kwenye Insta Story yake msanii huyo ameandika kuwa ni kweli walipata Ajali lakini kwa sasa wapo salama ikizingatiwa kuwa hawakupata majeraha mabaya.
Utakumbuka usiku wa kuamkia Februari 26 wasanii wa Mbuzi Gang walijaza nyomi la mashabiki katika ukumbi wa Alva Resort huko Maseno ambako walipiga show ya kufa mtu iliyowaacha mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka burudani zaidi.