Gossip

T-SHIRT YA BEI GHALI YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI NCHINI RINGTONE YAZUA GUMZO MTANDAONI

T-SHIRT YA BEI GHALI YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI NCHINI RINGTONE YAZUA GUMZO MTANDAONI

Watumiaji wa mitandao ya Kijamii nchini wamemtolea uvivu Staa wa muziki wa Injili  Ringtone Apoko baada msanii huyo kujigamba kuwa anamiliki T-Shirt ya bei ghali aliyodai kuwa ameinunua kwa shilingi milioni moja za Kenya.

Kupitia mitandao yao ya kijamii wamemtaka Mwanamuziki huyo akome kuishi maisha ya kuigiza na kuwahada Wakenya kwa kiki zisizo kuwa na mashiko kwani  T-Shirt yake hiyo ni batili.

Aidha wameenda mbali zaidi na kumtaka ringtone ache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wake na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye suala la kutoa muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe.

Kauli hiyo ya wakenya imekuja mara baada ya ringtone apoko kusikika kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni akijinadi kuwa licha ya kwamba anamiliki T-Shirt ya shilling millioni moja za Kenya bado ameokoka na anafuata misingi yote ya dini ya Kikristo tofauti na watu ambao vitu vya dunia huwachanganya na kuwapelekea kujihusisha na usherati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *