
Baada ya Diamond Platnumz kusogeza mbele kuachia Extended Playlist yake ya FOA Machi 11 ,mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize nae amesogeza mbele zoezi la kuachia wimbo wake mpya ambao utatoka machi 12.
Awali Diamond alitaja kuachia EP yake machi siku moja kabla ya tamasha la Afro East Carnival ambapo Harmonize nae alijibu mapigo kwa kutangaza kuachia wimbo mpya siku hiyo.
Hata hivyo ushindani huo haikuishia hapo kwani licha ya diamond platnumz kusogeza mbele tarehe ya kuachia EP yake mwanamuziki Harmonize pia amesogeza mbele tarehe ya kutoa wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Bakhresa’ na sasa utatoka machi 12, siku moja baada ya kutoka kwa FOA The EP ya mtu mzima Diamond Platnumz .