
Rapa kutoka nchini Marekani Snoop Dogg amethitibisha kwamba sasa anamiliki masters (nakala asili) ya album maarufu ya Dr. Dre “Chronic” ambayo ilitoka chini ya Death Row Records.
Hii imekuja kufuatia hivi karibuni kuanika wazi kuwa ameinunua label hiyo kongwe ya muziki.
Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali, dili la Snoop Dogg kuinunua Death Row Records halijawekwa wazi lakini inasemekana atakuwa na umiliki wa baadhi ya kazi zilizotoka chini ya label hiyo ikiwemo pia za marehemu Tupac Shakur.