
Album ya msanii Ali Kiba “Only One King” imefanikiwa kufikisha streams zaidi ya milioni 150.
Mauzo ya album hiyo ya yamebainishwa na meneja wa msanii Ali kiba, Aidan Charlie akimjibu shabiki aliyetaka kujua sababu ya “Only One King” kutofanya vizuri katika majukwaa ya kusikiliza muziki mtandaoni.
Shabiki huyo aliuliza kwenye sehemu ya comment, “Why isn’t it selling well on platforms if is a great album?” Aidan alilijibu swali hilo kwa kutoa takwimu za mauzo yake. “Tangu oktoba 7 hadi sasa, (Only One King) ina streams zaidi ya Million 150+ kwenye majukwaa yote ya kusikiliza muziki” – ameeleza Aidan.
Ikumbukwe album ya “Only One King” ilitoka Oktoba 7 mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 16 ya moto, na ni album ya tatu kwa mtu mzima ali kiba, baada ya Cinderella ya mwaka wa 2007 na Ali K for Real ya mwaka wa 2009.