Entertainment

ERIC OMONDI ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA WANAMUZIKI WA KENYA

ERIC OMONDI ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA WANAMUZIKI WA KENYA

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ametangaza ujio na tamasha la muziki ambalo litakuwa mahususi kwa wasanii wa Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eric Omondi, amethibitisha kuja na tamasha liitwalo “The Fill Up 254” ambalo litafanyika katika uwanja wa Carnivore, Aprili 2 mwaka huu.

Omondi ameeleza kwamba amekuwa akipigania muziki wa Kenya kwa muda sasa na wakati umewadia wa kutekeleza mabadiliko anayotaka kuyaona kwenye kiwanda cha muziki nchini.

Hata hivyo kupitia ukurasa rasmi wa tamasha hilo kwenye mtandao wa Instagram, majina ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la  “The Fill Up 254” yametajwa ambapo kundi la muziki wa Hiphop nchini Wakadinali limejumuhishwa kwenye orodha hiyo.

Ikumbukwe Eric Omondi amekuwa mstari wa mbele kutetea muziki na wanamuziki wa Kenya kwa kuhimiza vyombo vya habari kucheza kwa kiasi kikubwa nyimbo za wanamuziki wa ndani lakini pia amekuwa akishinikiza wanaoandaa matamasha nchini Kenya kuzingatia wasanii wa ndani badala ya kuwapa kipaumbele wasanii wa kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *