
Rapper kutoka Marekani Kanye West ameondolewa kwenye orodha ya Wasanii waliokuwa wamepangwa kutumbuiza kwenye ugawaji wa Tuzo za Grammy huko Las Vegas wiki mbili zijazo.
Msemaji wa Kanye West amesema walipokea simu kutoka kwenye Academy kuwajulisha kuwa rapa huyo ameondolewa kwa sababu inayotajwa kuwa ni kuhusu tabia zake za mtandaoni.
Mitandao ya Marekani imeripoti kwamba timu ya Kanye West haikushangazwa na uamuzi huo kutokana na Msanii huyo mwenye msimamo mkali kugonga vichwa vya habari kwa matukio yake ya hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ambayo yalisababisha hadi akafungiwa akaunti yake ya Instagram kwa kukiuka sera za Mtandao huo.
Kanye West ana shutuma za kutumia Instagram yake kuwapiga picha Watu kadhaa maarufu akiwemo Mke wake waliyeachana Kim Kardashian na mpenzi wake mpya Pete Davidson na pia alitumia Instagram yake kumkashifu Trevor Noah kwa kuzungumzia matukio yake kwenye kipindi chake cha The Daily Show.