
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Guardian Angel na mke wake Esther musila wamezindua jukwaa lao la kustream video za muziki
Jukwaa hilo liitwalo Solution.co.ke litatoa fursa kwa wasanii wa kenya na watengeneza maudhui kuingiza kipato kupitia maudhui wanayopakia kupitia mtandao kwa gharamu nafuu sana tofauti na majukwaa mengine kama Youtube
Hata hivyo Guardian Angel amesema hivi karibuni atatoa muongozo wa namna ambavyo wanamuziki na wabunifu watakavyowasilisha kazi zao kwenye mtandao.
Tayari couple hiyo imepakia video ya harusi yao na video ya wimbo mpya wa Guardian Angel uitwao money kwenye mtandao huo.