Entertainment

DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UZINDUZI WA VIDEO ZA FOA EP JUMATANO HII

DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UZINDUZI WA VIDEO ZA FOA EP JUMATANO HII

Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametangaza rasmi uwepo wa tukio la uzinduzi wa video za nyimbo zote kumi zinazopatikana kwenye EP yake ya “First Of All”

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa uzinduzi huo AMBAO NI kwa waalikwa tu utafanyika Machi 23,, Mlimani City jijini Dar es salaam

“23. 03. 2022 #FOA VIDEOS PREMIERE! Cinemax Mlimani City, Invitees Only! Everything is Different in #FOAtheEP” – ameandika Diamond Platnumz

Kando na hayo, ukiachilia mbali rekodi mbalimbali alizowahi kuweka Diamond, EP hiyo yenye mafanikio makubwa imeweza kuingiza nyimbo zake zote 10 zilizopo kwenye trending Youtube.

Ikumbukwe Diamond aliachia rasmi EP hiyo Machi 11, mwaka 2022 na mpaka sasa imefikisha streams zaidi ya milioni 30 kwenye platforms tofauti za kusikilizia muziki mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *