Entertainment

AKOTHEE ARUDI SHULE KUPATA SHAHADA

AKOTHEE ARUDI SHULE KUPATA SHAHADA

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee ameweka wazi kwamba amerejea shuleni kuendeleza masomo yake ili kupata shahada.

Mama huyo wa watoto watano amesema anatia bidii kubwa masomoni ili kumfanya mama yake ajivunie kumzaa mtoto kama yeye.

“Nilipotakiwa kuwa shuleni, niliamua kuwa mke, sasa badala ya kuwa mke, niko shuleni nikiwa na umri mkubwa maisha, haya maisha hayawi sawa kabisa” amesema.

“Lakini lazima nipate Shahada yangu kwa sababu ya mama yangu ili afurahie kuwa na kofia hiyo nyumbani kwake,” amesema Akothee kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Utakumbuka Akothee anataka kuwa miongoni mwa wasanii matajiri sana nchini Kenya ambapo utajiri wake unakadiriwa kufikia Dola10 Milioni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *