Entertainment

SAMA SOJAH AFUNGUKA KUWA MSANII HAWEZI TOKA KIMUZIKI BILA KUTOA KIINUA MGONGO KWA VYOMBO VYA HABARI

SAMA SOJAH AFUNGUKA KUWA MSANII HAWEZI TOKA KIMUZIKI BILA KUTOA KIINUA MGONGO KWA VYOMBO VYA HABARI

Msanii wa lebo ya muziki ya Redzone Music, Sama Sojah amefunguka na kudai kwamba msanii hawezi kutoka kimuziki hazipotoa kiinua mgongo kwa vituo vya redio na runinga zipige nyimbo zake.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni mwanamuziki huyo kutoka nchini Uganda amesema kwa miaka mingi muziki wake haujakuwa ukipata mapokezi mazuri kutokana kwa mashabiki kwa sababu alikuwa na mawazo hasi dhidi ya kulipa vyombo vya habari kucheza nyimbo zake, jambo ambalo amedai kwamba limemuathiri pakubwa kimuziki.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Cinderella” ametoa changamoto kwa wasanii chipukizi kutenga bajeti ya kurudisha fadhila kwa vyombo vya habari pindi wanapoachia nyimbo kama njia moja ya kuwatia moyo watangazaji na madeejay kupiga nyimbo zao kwani kipaji pekee hakitoshi kumsaidia msanii kutanua wigo wa muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *