Entertainment

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LASITISHWA RASMI BAADA YA MIAKA 19

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LASITISHWA RASMI BAADA YA MIAKA 19

Tamasha maarufu la utamaduni na muziki wa kiafrika, Sauti za Busara limesitishwa rasmi.

Baada ya miaka 19 ya kusherehekea tamasha hilo visiwani Zanzibar, Busara Promotions imetangaza kusitisha shughuli zake ifikapo Machi 31, mwaka 2022 kutokana na ukosefu wa rasimali na fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Unguja, mwanzilishi na Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud, amesema bila fedha za kulipa gharama za ofisi au mishahara tamasha hilo haliwezi kuendelea tena.

Tamasha la Sauti za Busara lilianzishwa machi mwaka wa 2003, na ni moja ya tamasha linaloongoza Barani Afrika kwa kutangaza na kusherehekea muziki na urithi wa kitamaduni wa kiafrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *