
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ujio wa ziara ya dunia kwa ajili ya kuitamgaza EP yake ya First Of All katika mataifa mbali mbali.
Diamond amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameipa ziara hiyo jina la FOA World Tour na inatarajiwa kuanza rasmi mwezi Mei’ mpaka Novemba mwaka huu. mahsusi kwa ajili ya FOA The EP pekee.
Tour hiyo itaanza Mei 7, huko Ethiopia na kumalizika Novemba 26, mwaka 2022 nchini Sierra Leone.
Katika taarifa yake Diamond Platnumz ameongeza kuwa ataendelea kutangaza tarehe za Ziara yake hiyo katika nchi Zingine.
Ikumbukwe Diamond aliachia rasmi EP hiyo Machi 11, mwaka 2022 na mpaka sasa imefikisha streams zaidi ya milioni 30 kwenye platforms tofauti za kusikilizia muziki.