Entertainment

KANYE WEST AJIONDOA RASMI KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

KANYE WEST AJIONDOA RASMI KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

Rapa kutoka Marekani Kanye West hatotumbuiza kwenye Tamasha la Coachella mwaka huu. Rapa huyo ameripotiwa kujiondoa kwenye orodha ya watumbuizaji wa tamasha hilo huku akiwa msanii kinara.

Wakati mashabiki wakiwa bado na maswali juu ya uamuzi huo wa Kanye West, Rapa Travis Scott naye ambaye angeungana na YE Jukwaani, hatokuwepo kwenye tamasha hilo linaloanza wikendi ijayo huko Indio, California.

Bado haijafahamika sababu hasa ya Kanye West kujiondoa, lakini kiuhalisia alikuwa na mwezi mgumu sana, akishambuliana mitandaoni na Kim Kardashian pamoja na Pete Davidson.

Lakini pia  sakata lake na Trevor Noah lililomfanya kuondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa Tuzo za Grammy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *