
Rapa Breeder LW ameshindwa kuzuia hisia zake za mahaba kwa malkia wa tiktok Azziad pamoja na mchekeshaji Cartoon Comedian kwa kueleza wazi kuwa anawapenda sana.
Breeder amefafanua kuwa ameamua kuwa mkweli na muwazi kwani warembo hao wana sifa zote anazozitafuta kwa mwanamke wa ndoto yake ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yuko tayari kumuoa mmoja kati yao endapo akikubali ombi lake.
Rapa huyo ameweka wazi hayo alipokuwa akimjibu shabiki yake ambaye alitaka kujua ni warembo wagani hapa Kenya anatamani kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi katika kikao cha maswali na majibu kupitia mtandao wa Instagram.