
Staa wa muziki nchini Akothee amelamba dili nono la kuwa balozi wa kampuni ya Unga Limited ambayo inazalisha unga wa ugali,uji na ngano.
Akothee ametengaza habari njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Unga limited.
Lakini pia ameishikuru uongozi wa kampuni ya Unga limited kwa kutambua nguvu yake na kuhamua kumpatia dili hilo ambalo litamjengea heshima.
Hata hivyo kampuni ya Unga Limited imesema imeingia ubia kufanya kazi na Akothee kwa sababu ya ubunifu, bidii pamoja na ushawishi wake kwenye jamii huku ikisema kwamba wana imani msanii huyo ataingozea kampuni hiyo wateja wengi zaidi.
Akothee sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Unga limited kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongeza mauzo ya unga hiyo ya ugali, uji na ngano.