Entertainment

H_ART THE BAND WATAMBULISHA COVER LA ALBUM YAO MPYA

H_ART THE BAND WATAMBULISHA COVER LA ALBUM YAO MPYA

Kundi la muziki nchini Hart the Band limetambulisha rasmi cover la album yao mpya iitwayo Party Time.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limechapisha cover ya album yao huku likisema album hiyo itatoka rasmi Mei 6 mwaka huu wa 2022.

Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021.

Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *