Entertainment

AKOTHEE AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO

AKOTHEE AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO

Mwanamuziki maarufu nchini Akothee amefunguka safari ya kupambana na msongo wa mawazo ikiwa ni siku chache imepita baada ya kufikisha umri wa miaka 41.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee ameeleza kuwa amekuwa aking’ang’ana na msongo wa mawazo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita huku akiwahimiza wanaokumbana matatizo hayo ya afya ya akili kujitokeza na kuzungumzia hali zao kwa watu wao karibu ili waweze kupata usaidizi.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sweet Love” ametoa angalizo kwa jamii kutochukulia matatizo ya afya ya akili kwa mzaha huku akisema kwa sasa anafurahia jinsi hali yake ya afya ya akili inazidi kuhimarika.

Utakumbuka Mwezi Septemba mwaka wa 2021 Mwimbaji huyo alitasanua kuwa amekuwa akipambana na hofu ya kuwa mtu maarufu ambapo alienda mbali zaidi na kukiri kuwa ilifika pahali alianza kuwaepuka mashabiki zake kiasi cha kujuta kuwa na umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *