
Nyota wa muziki kutoka nchini Uganda Cindy Sanyu amefunguka chanzo cha migawanyiko miongoni mwa wasanii nchini humo.
Katika mahojiano yake hivi karibuni, Cindy amesema siasa imesabaratisha juhudi za kuunganisha wasanii nchini Uganda kwa kuwa baadhi ya wasanii wanafanya maamuzi yao kulingana na itakadi za kisiasa ya vyama wanavyoshabikia.
Hata hivyo amesema licha ya yeye kuweka mikakati ya kuwaleta wasanii pamoja kupitia muungano wa UMA, imekuwa vigumu kwake kufanikisha jambo hilo kutokana na siasa, jambo ambalo amedai ni changamoto ambayo alikumbana kipindi anahudumu kama rais wa muungano huo.
Cindy Sanyu atachuana na King Saha, Maurice Kirya kwenye kinyanganyiro cha kugombea urais wa muungano wa wasanii nchini uganda kwenye uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.