
Hatimaye Rapa kutoka nchini Kenya Boutross ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Yea Yea Yea” amewabarki mashabiki zake na “Kabla Mtindo” , EP ambayo ina jumla ya nyimbo 8 za moto, ikiwa na kolabo 7 pekee kutoka kwa wakali kama Chinbees, Ndovu Kuu,Barack Jacuzzi, Munyax,na wengine wengi.
EP hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Uchi Wale, Mwanangu,Sweety, Confuse Me na nyingine nyingine.
Hii ni EP ya tatu kwa mtu mzima Boutross, tangu aanze safari yake ya muziki baada ya 6IX ya mwaka wa 2019 na Billy Jean ya mwaka wa 2018.
Lakini pia ana 6ixviewsii8k mixtape iliyotoka mwaka wa 2020 ikiwa na juma ya mikwaju ya 24 ya moto