Entertainment

JOVIAL AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUFANYA KAZI NA OXLADE KUTOKA NIGERIA

JOVIAL AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUFANYA KAZI NA OXLADE KUTOKA NIGERIA

Msanii wa kike nchini Jovial amedokeza mpango wa kufanya kazi ya pamoja na mwanamuziki kutoka nigeria Oxlade.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema anatamani kushirikiana na Oxlade kwenye wimbo wa pamoja kwa kuwa  yeye ni shabiki mkubwa wa hitmaker huyo wa ngoma ya Ojuju .

Ujumbe ambao umewaaminisha watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii huenda wawili hao wana wimbo wa pamoja ambao utatoka hivi karibuni.

Utakumbuka mapema mwaka huu Jovial aliweka wazi kwamba hatofanya kolabo na msanii yeyote kwa kuwa ameshashirikisha na wasanii wengine kwenye nyimbo zao hivyo ni wakati wake wa kuachia nyimbo zake mwenyewe kama msanii wa kujitegemea licha ya kupokea maombi mengi.

Hata hivyo alienda mbali zaidi na kusema kolabo ambazo zitatoka mwaka huu alizoshirikishwa na wasanii wengine ni zile alizofanya mwaka jana.

Jovial ambaye anafanya vizuri na wimbo wa Mi Amor alioshirikishwa na Marioo tayari ameshirikiana na wasanii kama Mejja, Khaligraph Jones, Arrow Boy, Otile Brown na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *