
Msanii aliyegeukia siasa Jaguar amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kwenye mchujo wa kumchagua mgombea wa ubunge katika eneo la Starehe kupitia Chama cha UDA.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jaguar ameonekana kutokubali ushindi wa Simon Mbugua ambaye alimshinda kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama cha UDA uliofanyika Aprili 21 kwa kusema kwamba uchaguzi huo wa mchujo ulikumbwa na udanganyifu mwingi huku akimiri hadharani kwamba alitabiri ushindi wa mbugua baada ya cheti chake cha uteuzi kusambaa mtandaoni hata kabla ya uchaguzi haujafanyika.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kigeugeu” amesema atatoa mweelekeo atakaochukua hivi karibuni baada ya kufanya mkao wa pamoja na wakaazi wa Starehe ikizingatiwa kuwa wakaazi wa eneo bunge lake wamenyimwa haki yao ya kumchagua kiongozi wanaempenda.
Hata hivyo wakenya wametoa mitazamo tofauti kuhusu kushindwa kwa jaguar ambapo baadhi wamemtaka msanii huyo akubali ameshindwa kwenye mchujo wa uda huku wengine wakisema kwamba masaibu yanayomuandama yametokana na yeye kuikimbia chama cha jubillee ambacho kilimpeleka mbungeni.
Utakumbuka kwenye mchujo wa kwanza Jaguar alishindwa na Simon Mbugua jambo lilompelekea kukataa rufaa ya kuandaliwa kwa uchaguzi mwingine kwa kuwa ulikumbwa na dosari nyingi.