Entertainment

AKOTHEE AWATOLEA UVIVU WANAOFURAHIA ANGUKO LAKE

AKOTHEE AWATOLEA UVIVU WANAOFURAHIA ANGUKO LAKE

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amekanusha madai ya kuachana na mpenzi wake Nelly Oaks mara baada ya kuandika ujumbe uliotafsiriwa na wengi kuwa huenda penzi lao limefikia kikomo.

Kupitia instagram Akothee ameshangazwa na kitendo cha watu kufurahia anguko lake huku akidai kwamba chapisho lake lilikuwa mzaha.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahishwa na hatua ya Akothee kuwadanganya wafuasi wake huku wengine wakidai kuwa msanii huyo anatafuta Β mazingira ya kuzungumziwa na wanablogu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *