Entertainment

SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa muziki a Bongofleva Diamond Platnumz anatarajia kuachia album yake ya nne katika maisha yake ya muziki baada ya kupata mafanikio makubwa na album ya ‘A Boy From Tandale’ mwaka wa 2017.

Akizungumzia ujio wa album hiyo, amemtaja producer mkubwa wa muziki kutoka Marekani Swizz Beatz kuwa ndio mtayarishaji mkuu wa album yake ijayo (executive producer).

Diamond ameeleza hayo akiwa nchini Uingereza kupitia Podcast ya Afrobeats inayoongozwa na Adesope.

Huu unakuwa ni muendelezo wa Swizz Beatz kufanya kazi pamoja na Diamond, hivyo kumfanya mkali huyo wa wonder kuwa msanii wa kwanza Afrika kutayarishiwa album na Swizz Beatz.

Mwaka 2020 Diamond Platnumz alishirikishwa kwenye album ya Alicia Keys, ‘ALICIA’ na kusikika kwenye wimbo uitwao Wasted Energy. Album hiyo ya Alicia ilitayarishwa na mumewe Swizz Beatz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *