
Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ametaja Jina la Album yake mpya anayotarajia kuachia hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kaa La Moto ameshare cover ya album yake mpya na kutusanua kuwa album yake hiyo ambayo anaiandaa chini studio za Kubwa Studios mjini mombasa Itaitwa LESO YA MEKATILILI.
Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yake ya LESO YA MEKATILILI, Hitmaker huyo wa Dear Hihop hajatuambia tarehe ambayo album hiyo itaingia sokoni rasmi. ila ni jambo la kusubiriwa.
Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto baada ya kesi ya mwaka wa 2019