Entertainment

BAHATI AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA BUNGE MATHARE KAMA MGOMBEA HURU

Staa wa muziki nchini Bahati ameweka wazi kuwa hatagombea kama mgombea binafsi kwenye kinyanganyiro cha ubunge wa mathare, siku chache baada ya kuangua kilio aliposhurutishwa na chama cha jubilee kujiuzulu wadhfa wa ubunge kwa ajili ya kumpa nafasi mbunge wa sasa tom olouch.

Bahati amesema atakuwa amekisaliti chama chake cha Jubilee akiwania kiti ubunge mathare kama mgombea huru, jambo ambalo amedai hayuko tayari kukifanya.

Katika mahojiano na Radio Maisha, Bahati hata hivyo ameshikilia kuwa bado ana Cheti chake cha Uteuzi na ana matumaini kuwa jina lake litawasilishwa kwa tume ya uchaguzi  IEBC leo.

‘Naweza kukuambia kitu? Unajua kwangu, sina haja na kuwa mgombea huru, kwa sababu nahisi hiyo ni kama kukisaliti chama changu na ninaamini pia chama hakitasaliti watu wao… kwa sababu … kina nafasi kwa vijana …’’ Bahati alisema.

Msanii huyo aliyelelewa Mathare hata hivyo amesema kuwa amefanya mazungumzo na chama hicho baada ya kutakiwa kurejesha Cheti chake na hivyo amewatolea hofu wafuasi wake kuwa mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni.

“Mgombea wangu…waliitisha mkutano … nilifikiri chama kilitaka kunifadhili, lakini waliniomba nijiuzulu kama mgombea wa ubunge mathare kwa ajili ya mbunge wa sasa… Wanajua mashinani mambo yamebadilika… nimefanya mazungumzo upya na chama …” alifichua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *