
Msanii kutoka nchini Kenya Gabiro mtu necessary ameachia rasmi album yake mpya “Saint John” ambayo mashabiki zake wamekuwa wakisubiri kwa hamu.
“Saint John” ina jumla ya ngoma 11 za moto huku ikiwa na collabo 2 kutoka kwa wakali kama Blak Angel na Javada.
Album hiyo ambayo ina ngoma kama kula bata, happy, Dear son, inapatikana exclusive kwenye digital platform zote za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni kama vile Boomplay Kenya na Spotify.
Saint John ni Album Ya Kwanza kwa Gabiro Mtu Necesary ,ikizingatiwa kuwa Tayari ana Ep Mbili Alizoachia mwaka mwaka wa 2020 na 2021 mtawalia ambazo ni Jenesis, na Mpito.