Sports news

BARCELONA KUTOTUMIA CAMP NOU MSIMU WA 2023-24

BARCELONA KUTOTUMIA CAMP NOU MSIMU WA 2023-24

Klabu ya Barcelona imethibitisha kufanyia marekebisho ya uwanja wa Camp Nou na wametangaza kuwa timu hiyo msimu wa 2023-24 itatumia uwanja wa Olympic kwenye eneo la Montjuic ndani ya jiji hilo.

Uboreshaji utaanza mwezi Juni, baada ya kumalizaka kwa msimu huu, baada ya bodi kuthibitisha kiasi cha €1.5 billion ili kuweza kufanya maboresho ya uwanja huo maarufu duniani.

Inatarajia kuwa maboresho yatachukua miaka minne kwa kazi zote kumalizika, hii inamaanisha kuwa Barcelona watapaswa kuhama kwa msimu ujao na kuhamia kwenye uwanja wa Olympic ambao unatumika na timu ya Espanyol.

Klabu ya Barcelona itaweza kuutumia uwanja wa Camp Nuo kwa msimu unaofuata, baada ya msimu 2023-24, huku wakitarajiwa kupunguza idadi ya watazamaji kwa asilimia 50 kwa sababu za ujenzi.

“Kitakuwa kiwanja bora duniani, ndani ya jiji bora duniani, ndani ya nchi bora duniani” – ameeleza Joan Laporta, Rais Barcelona akiiambia radio ya huko Catalan, RAC1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *