
Staa wa muziki nchini Jovial ameshindwa kumvumilia shabiki yake mmoja ambaye amemkosesha amani kwa kudai kuwa ana mapenzi dhati kwake.
Kupitia instastory kwenye mtandao wa instagram jovial amesema shabiki huyo ameenda mbali zaidi na kuanza kuwalipa watu kumfuatilia sehemu anayoishi na maeneo anayotembea.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe Remix” amesema amejaribu kumu-block mtu huyo na hata kumtishia atampeleka polisi lakini ameshindwa kubadilisha mienendo ya shabiki huyo ambaye anadai anampenda kwa dhati.
Hata hivyo amewataka mashabiki zake wamsaidie kumkomesha shabiki huyo msumbufu huku akisema amechoka kukaa kimya kwani jambo hilo limeanza kumpa uwoga katika maisha yake.