Entertainment

KANYE WEST ASHTAKIWA KWA WIZI WA AUDIO

KANYE WEST ASHTAKIWA KWA WIZI WA AUDIO

Rappa kutoka Marekani Kanye West ameripotiwa kushtakiwa na Askofu David Paul Moten kutoka Texas kwa madai ya ku-sample moja kati ya audio ya mahubiri yake na kuitumia katika ngoma yake ya “Come To Life” inayopatikana kwenye album ya Donda bila ya ridhaa yake.

Katika nyaraka zilizodakwa na TMZ, Askofu Paul Moten anadai kuwa mahubiri yake yalitumika kwa muda wa sekunde 70 katika ngoma hiyo yenye dakika 5 na sekunde 10, ambayo ni zaidi ya asilimia 20 ya wimbo huo.

Askofu David Paul Moten pia amezishtaki , lebo za Universal Music Group, Def Jam pamoja na Good Music katika msala huo, hivyo anadai fidia alipwe na pande zote hizo nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *