
Rapa kike nchini noti flow amesikitishwa na kitendo cha mpenzi wake king alami kushiriki kwenye biashara ya ngono mtandaoni licha ya kumhakikisha kuwa atafuta akaunti yake aliyofungua kwenye tovuti moja.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram noti flow amesema ameumizwa na hatua ya mpenzi wake huyo kufuta akaunti aliyokuwa anaijua na kisha akafungua akaunti nyingine kwenye mtandao mmmoja wa biashara ya ngono bila ufahamu wake.
Noti Flow ameenda mbali zaidi na kusema kwamba Alami amechapisha picha zake walizozipiga kipindi cha uchumba wao kwenye ukurasa wake mpya wa tovuti ya biashara ya ukahaba aliyofungua majuzi.
Kulingana na Noti Flow, tabia hiyo imemfanya aamue kutomsamehe Alami, licha ya kutaka kumsamehe kutoka kitendo chake cha nyuma cha kutoka kimapenzi na mwanaume mmoja tajiri.
“Woow… Nilikuwa nikifikiria kukusamehe lakini sasa… Karibu Kanairo ambapo unampelekampenzi wako kwenye mtoko na kumpiga picha ili yeye tu azitumie picha hizo kwenye tovuti ya ukahaba,” Noti Flow aliandika kwenye Instagram yake.
Hata hivyo, imekuja siku chache baada ya Alami kumuandikia noti flow ujumbe mzito wa mapenzi kupitia ukurasa wake wa Instagram akisindikiza na jina la Noti Flow.
“Kuna wakati utaniudhi na kunisababishia hasira zisizohitajika, lakini hata iweje, nitakupenda daima. Kuna maneno ya kikatili unaweza kusema ambayo yataniumiza na kuniletea huzuni…Katika maisha, kuna mapambano, mabishano na changamoto ambazo tutalazimika kuvumilia lakini haijalishi nini kitatokea… Ninaweza kuwa nalia sasa lakini niko sawa,” Ujumbe wa Alami ulioandikwa kwa mkono umesomeka