Entertainment

VDJ JONES AMVUA NGUO MADOXX WA BOONDOCKS GANG, ADAI MIHADARATI IMEATHIRI UTENDAKAZI WAKE

VDJ JONES AMVUA NGUO MADOXX WA BOONDOCKS GANG, ADAI MIHADARATI IMEATHIRI UTENDAKAZI WAKE

DJ maarufu nchini VDJ Jones amepuzilia mbali madai kuwa msanii wa Boondocks gang Edu Madoxx anapitia wakati mgumu siku chache baada ya msanii huyo kujitokeza na kuomba msaada wa kodi kutoka kwa wakenya.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Vdj Jones ambaye ni muasisi wa muziki wa gengetone amefichua tusiyoyajua kuhusu Madoxx kwa kusema kwamba madawa ya kulevya yameponza msanii huyo kiasi cha kuwafanya wasanii wenzake Exray pamoja na Odi wa Murang’a kumkimbia.

Vdj Jones ameenda mbali zaidi na kusema kuwa msanii huyo amekuwa akitumia mihadarati kwa kipindi kirefu  jambo analodai limemuathiria kiafya na hata kumpelekea kuzembea kwenye suala la kufanya kazi katika kundi la Boondocks gang.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao wa kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Vdj Jones wengi wakimtaka aache suala la kutoa lawama kwa msanii huyo na badala yake ashirikiane na mashabiki wamsaidia madox ambaye wakenya wengi wamehoji kuwa huenda anapitia msongo wa mawazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *