
Msanii wa Bongofleva Beka Flavour ameachia rasmi Album yake mpya inayokwenda kwa jina la First Born.
Album hiyo ambayo inapatikana exclusive kupitia Boomplay ina jumla ya ngoma 15 ya moto huku ikiwa na kolabo 7 pekee.
Beka flavour amewashirikisha wakali kama Barnaba, Christian Bella, Naiboi, Linah, Young Lunya, na Yamoto Band huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Wivu, Medula, Dunia Tunapita na nyingine nyingi.
First Born ni album ya kwanza kwa mtu mzima Beka flavour kuitoa tangu aanze safari yake ya muziki.