Entertainment

CAROL NANTONGO AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BENDI YA MUZIKI YA GOLDEN

CAROL NANTONGO AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BENDI YA MUZIKI YA GOLDEN

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Carol Nantongo amefunguka sababu iliyofanya kujiondoa kwenye bendi ya muziki ya Golden.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Carol Nantongo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya “Oliwa” amesema bendi hiyo haikuwa na mazingira mazuri ya kufanyia muziki kwa sababu wanachama wake walianza kuchanganya kazi na siasa.

Mwaka wa 2020 Carol Nantongo alijiondoa kwenye bendi ya Golden na akaanza kufanya muziki kama msanii wa kujitegemea.

Golden Band ambayo ilikuwa chini Eagles Production ilikuwa inaundwa na wasanii kama Ronald Mayinja, Catherine Kusasira, Fred Sseruga, Stecia Mayanja na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *