
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Foby ameshindwa kabisa kuficha hisia zake kwa Mrembo Zuchu kutoka WCB.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Foby ameamua kuonesha hisia zake kwa Zuchu kwa kuweka jumbe mbalimbali zikielezea jinsi Anamzimia.
Foby amebainisha kuwa kuna kipindi aliishi kwa ugumu baada ya kusambaa kwa taarifa zikidai Zuchu anataka kuolewa.
Hata hivyo ameomba kuwepo na Wizara ya Mahusiano akihofia kuumia na kuja kufa kwa kulikosa penzi la mrembo huyo.
“Hakuna kipindi nimeishi kwa ugumu kama kile kipindi wanasema anataka kuolewa,Roho yangu ilikuwa kama ya kuazima,Mi niliamua kum_Unfollow kwasababu nikiona picha yake tu mshtuko naoupata utasema nipo nchi ya ukrain,
kwani hakuna wizara yoyote inayoweza kupatanisha watu nchini kwetu? Pls kuwe na wizara ya mahusiano na mapenzi haki vile kuna watu tunaumia na tutakuja kufa tumesimama,
Nyie huyu mtoto mi atakuja kuniua huyu,” Ameandika FOBY kupitia Instagram.
Hajajulikana kama kweli Foby anahusudu penzi la zuchu au anatumia jina lake kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.