
Msaniii kike nchini Nadia Mukami amewashauri kwa akina mama wa chang kukubali usaidizi pindi wanapohitaji wakiwa kwenye harakati za kuwalea wanao.
Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram na Mashabiki zake Nadia amesema hatua hiyo itasaidia kuondokana na matatizo ya afya akili yanatokana na malezi ya watoto.
Katika hatua nyingine Nadia Mukami ametoa changamoto kwa vijana kujipanga kiuchumi kabla kuwapata watoto kwani majukumu ya malezi sio mapesi kama wengi wanavyodhani.
Kauli ya Nadia Mukami inakuja mara baada ya kuweka wazi kuwa ameongeza uzito kutoka kilo 55 hadi 63 kutokana kula chakula kingi kwa ajili ya kupata maziwa ya kumnyonyesha mtoto wake Hasib Kai ambaye ana umri wa miezi miwili.