
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana inaonekana hataki kabisa kulaza damu kwenye suala la kuupeleka muziki wake kimataifa.
Msanii huyo wa Source Managemnent ambaye ameamua kuwapuuza baadhi ya watu wanakosoa muziki wake, ametangaza kuwa yupo kwenye matayarisho ya mwisho kwa ajili ya kuja na tour yake ya muziki nchini uganda.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbikka” amesema tour hiyo ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuwapa mashabiki zake burudani, itang’oa nanga huko Mbale nchini Uganda kabla ya kuelekea kwenye miji mbali mbali nchini humo.
Utakumbuka Spice diana amegonga vichwa vya habari nchini Uganda kwa kipindi cha wiki mbili sasa mara baada ya kuachia StarGal EP yenye jumla ya singo 6 ya moto.
Utakumbuka juzi kati Pallaso amehitimisha tour yake ya kitaifa ambayo ameifanya kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita ndani miji 19 nchini Uganda