
Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amewaacha wafuasi wake na maswali mengi baada ya kukiri hadharani kuchoshwa na mapenzi.
Kupitia ukarasa wake Instagram Akothee amethibitisha kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Nelly Oaks huku akisema kwamba hatoweka wazi sababu za kuachana na mpenzi wake huyo .
Msanii huyo amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake zote kwenye muziki huku akiwataka wanablogu kutomuuliza maswali kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi.
Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutochukulia kwa uzito taarifa hiyo kwa kuwa mwanamama huyo amekuwa na mazoea ya kutangaza kuachana na Nelly Oaks mara kwa mara lakini baadae wanafuafua penzi lao.