
Hitmaker wa ngoma ya “Holiday”, Msanii Hope Kid amedokeza mpango wa kuzindua studio ya kurekodi muziki iitwayo Autism Lights.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Hopekid amesema studio hiyo ya muziki itakuwa mahususi kwa ajili ya kukukuza vipaji vya watoto wenye changamoto ya usonji (Autism).
Katika hatua nyingine Hope Kid pia ametusanua kuwa Juni 20 mwaka huu, watatembelea makazi ya watoto walioathirika na usonji ambapo watatoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine ya msingi, msaada ambao utawasaidia kujikimu kimaisha katika kipindi cha miezi 6 ijayo.
Usonji ni hali ambayo mtu huwa nayo tangu utotoni ambayo hutambulika kwa mhusika kushindwa kuwasiliana vizuri na pia kujihusisha na watu wengine katika mambo mbalimbali ya kijamii katika hali ya kawaida.