
Kundi la muziki nchini Sauti Sol wameingia ubia wa kufanya kazi na jukwaa la uwekezaji linakuja kwa kasi barani kwa jina la Ndovu tech.
Sauti sol wamethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa kusema kwamba ushirikiano wao na jukwaa hilo litawapa fursa ya kuhamasisha watu kuhusu umihimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kwenye masuala ya uwekezaji.
Hitmaker hao wa ngoma ya “Suzzana” wamesema dili hilo itatoa nafasi pia kwa mashabiki zao kufikia uhuru wao wa kifedha kwa kuwekeza kwa vitu vitakavyowaingizia kipato.
Hata hivyo Ndovu Tech ambayo ni jukwaa la uwekezaji linalotoa nafasi kwa watu kupata huduma za kifedha sokoni imewakaribisha sauti sol katika familia yao.