Entertainment

CHRIS BROWN AKIRI KUREKODI NYIMBO 250 KWA AJILI YA ALBUM YAKE MPYA

CHRIS BROWN AKIRI KUREKODI NYIMBO 250 KWA AJILI YA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown amefunguka kwamba alirekodi nyimbo 250 katika kipindi cha miaka mitatu ambayo alikuwa akiitayarisha Album yake mpya “Breezy” ambayo itaachiwa June 24 mwaka huu.

Katika nyimbo hizo 250 ilibidi zipunguzwe na kupatikana 23 ambazo zimetokea kwenye Tracklist ya Album hiyo.

Kwenye mahojiano na Big Boy TV, Breezy ameelezea mchakato wa kupunguza ngoma hizo ambapo amesema nyimbo nyingi zilikuwa zinafanana ‘sound’ hivyo ilimchukua muda kuchagua na kupata hizo 23 kwa ajili ya masikio ya mashabiki zake.

Album yake ya mwisho “Indigo” ya mwaka 2019 ilikuwa na Jumla ya nyimbo 32 na baadaye ziliongezwa nyimbo zingine na kufikia 42.

Chris Brown anafahamika kwa kuwa na maktaba ya  nyimbo nyingi, mwaka 2017 wakati aki-promote Album yake ‘Heartbreak on a Full Moon’ alimwambia Mtangazaji Ebro kwamba ana nyimbo 800 kwenye simu yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *